Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga waanza na ushindi dhidi ya Asas

IMG 5437 Musonda Goal.jpeg Mfungaji wa bao la Pili la Simba SC

Sun, 20 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, ASAS ya Djibouti katika mchezo wake wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yamefungwa na wachezaji wake wa kigeni, kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 22 na mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia, Kennedy Musonda dakika ya 53.

Timu hizo zitarudiana Agosti 26 hapo hapo Chamazi Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya kati ya Otoho ya Kongo Brazzaville na El Mereikh ya Sudan kuwania tiketi ya makundi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: