Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mmetisha, ila kazi bado

Yanga 0114 Yanga mmetisha, ila kazi bado

Tue, 16 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmeupiga mwingi sana vijana wa Jangwani, Yanga Afrika kama ambavyo mmekuwa mkijiita wenyewe.

Mmeipa heshima sana nchi hii na kama mtashikilia hapo mlipo basi historia mpya mtakwenda kuitengeneza.

Hakika mna kila sababu ya kupongezewa na kutembea kifua mbele kwa sasa wakati huu mkiwa mnafurahia zile chuma 2-0 mlizowapa Marumo Gallants kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Pamoja na ushindi huo tunawakumbusha kuwa, soka ni mchezo wa maajabu, huwezi kujiona umeshinda hadi pale filimbi ya mwamuzi itakapopigwa.

Hivyo Yanga hamtakiwi kujiona kama tayari mmefuzu fainali kwakuwa mnaongoza kwa mabao 2-0, tuseme ni hatua nzuri kwa dakika 45 za kwanza lakini zile dk 45 za pili huwa ngumu zaidi.

Watanzania tupo nyuma yenu, tunawaombea muweze kufanya maandalizi kabambe kabla ya kwenda kurudiana huko Afrika Kusini Mei 17 yaani Jumatano ijayo.

Wachezaji mkacheze kwa nidhamu na tahadhari kule Sauz, mafanikio ya Yanga ni ya taifa zima. Kwenye rekodi itatajwa Yanga ya Tanzania.

Marumo siyo wabaya, kama ambavyo tuliwaona wote hapa namna ambavyo walicheza, ni timu ambayo inaonekana kutojali, kama mkiweza kucheza na akili zao basi mtafanikiwa.

Mungu awabariki sana katika harakati zenu hizi za kutaka kuiweka kwenye ramani ya juu soka la Tanzania na ni jambo ambalo linalowezekana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: