Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga mambo magumu Fainali Shirikisho, wakubali kichapo kwa Mkapa

IMG 4176 Yanga 1 2 Usm.jpeg Yanga ikiwa nyumbani kwa Mkapa imekubali kichapo cha magoli

Sun, 28 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Timu ya Yanga imekubali kichapo cha magoli 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho.

Yanga walijikuta katika wakati mgumu dakika ya 32 tu ya mchezo baada ya kutanguliwa kwa bao la kichwa la Aimen Mahious.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinakamilika ni wageni USM Algiers ndio waliokwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa uongozi wa bao 1-0.

Kipindi cha pili Yanga walirudi kw kasi na wakafanya mabadiliko yaliyoleta uhai katika eneo lao la kiungo kwa kumuingiza Abubakar Salum "Sure Boy" aliechukua nafasi ya Aziz KI.

Dakika ya 82 Fiston Mayele aliwarudisha Yanga mchezoni kwa bao la kusawazisha akimalizia pasi safi ya kichwa ya Mudathir Yahya na kufikisha mabao 7 katika akiongoza orodha ya wafungaji Kombe la Shirikisho

Dakika 4 tu zilitosha kuwarudisha wageni katika uongozi baada ya Islam Merili kupachika bao la pili dakika ya 86 na kuwafanya wageni kuwa mbele kwa mabao 2-1.

Mpaka dakika 90 zinakamilika ni USM Algiers ndio walioondoka na ushindi na kujiweka katika mazingira mazuri ya kunyakua taji la Shirikisho.

Mchezo wa Fainali ya mkondo wa pili utapigwa June 3 nchini Algeria na Yanga watahitaji ushindi wa kuanzia angalau mabao 2-0 ili waweze kunyakua ubingwa.

Je Wananchi wataweza kupindua meza?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: