Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kushusha chuma kingine leo

Maxi Nzengeli Gd Yanga kushusha chuma kingine leo

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema leo ALhamisi, Julai 13, 2023 itatambulisha mchezaji mwingine mpya ambaye atajiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao.

Mpaka sasa Yanga imetambulisha wachezaji watatu ambao ni Nickson Kibabage (beki na winga kutoka Singida FG), Jonas Mkude (kiungo kutoka Simba Sc) na Gift Fred (beki kutoka SC Villa ya Uganda) huku akitajwa pia winga Maxi Nzengeli kutoka Maniema FC ya Congo DR kuwa huenda ndiye akatangazwa leo.

"Baada ya kutambulisha wachezaji watatu mpaka sasa, tunakwenda kuongeza wengine kwenye kikosi chetu na leo tutatambulisha chuma kingine, keshokutwa tena mpaka tutakapomfikia mtu wa mwishoa ambaye tumepanga kwenye utambulisho wetu.

"Tukimaliza hiyo sasa tunakuwa tumetambulisha kikosi chetu chote ambacho tutakuwa nacho msimu ujao. Nadhani mmeshaanza kuona picha wachezaji wetu wakiwa mazoezini.

"Tunaamini kwa kikosi hiki tutapata ushindani mzuri kwa Kaizer Chiefs na kuwajenga vizuri wachezaji wetu kuelekea kwenye Ligi na michuano ya kimataifa," amesema Ally Kamwe, Ofisa habari wa Klabu ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: