Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kumstaafisha Nonga

Nonga Picrr Yanga kumstaafisha Nonga

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa nahodha wa Mbeya City ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi, Paul Nonga anatarajia kutundika daruga kesho Jumanne Mei 6 katika mchezo dhidi ya Yanga.

Nonga anasema ameamua kutundika daruga katika mchezo huo sababu amezitumikia timu zote kwa nyakati tofauti akiwa mchezaji.

Amesema umekuwa wakati mwema kwangu katika soka na sasa ataonekana uwanjani kwa majukumu mengine na sio kama mchezaji.

"Nipende kumshuru Mungu kuniwezesha kufika hatua niliyonayo kwenye soka sababu sio wote wanamaliza salama safari yao ya soka kama mchezaji,”

"Pia niwashukuru viongozi wa Mbeya City kwa kunilea mkama mtoto wao katika nafasi ya mchezaji na kunisomesha ukocha hadi leo hii najivunia na kusimama mbele za watu," amesema Nonga.

Nonga ambaye wazazi wake walipenda awe mchungaji anasema hakuweza kutekeleza mapendekezo ya wazazi sababu asingefurahia kazi hiyo na ndiko jina la 'Baba Paroko' lilikoanzia.

Anasema sababu kubwa inayomfanya kuacha kucheza ni kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara hivyo akaona hataweza kudumu katika soka la ushindani.

Nonga alianza soka la ushindani JKT Oljoro kisha akajiunga na Mbeya City kisha akaenda Mwadui, Yanga, akarudi tena Mwadui, Lipuli, Gwambina na sasa Mbeya City.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: