Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kufungua matawi Congo DR

Yanga Kwa Mkapa 1 1140x640 Yanga kufungua matawi Congo DR

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga inaenda kuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufungua matawi ya klabu hiyo Nchini Dr Congo.

Wanachama wapya wa klabu hiyo Nchini DR Congo wameiomba klabu hiyo ikazindue matawi hayo watakapoenda kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya TP Mazembe.

Kwa mujibu wa katiba mpya ya Yanga, pamoja na vitu vingine tawi litakidhi vigezo kusajiliwa ikiwa limefikisha Wanachama (100), hivyo basi, matawi yaliyokidhi vigezo ambayo yatazinduliwa yatakuwa (3).

Klabu ya Yanga itaondoka nchini leo saa 5 asubuhi kuelekea DR Congo kwa kutumia ndege ya ATCL tayari kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa Aprili 2, 2023. Msafara mwingine ambao utaambatana na mashabiki utaondoka kwa basi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: