Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga kimya kimya kwa George Mpole

George Mpole Abadili Yanga kimya kimya kwa George Mpole

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga Sc imetambulisha wachezaji wapya watano hadi sasa ambapo watatu ni wa kigeni na wawili wazawa, lakini Kuna taarifa kuwa iko mbioni kushusha Mfungaji bora wa Ligi Kuu kwa msimu wa 2021/2022, George Mpole (30), anayekipiga ES Lupopo ya DR Congo kwa sasa.

Yanga imeonyesha nia ya kumtaka Mpole kwa mara ya pili na duru hii ni baada ya ligi ya DR Congo kusimama kwasababu ya machafuko yanayoendelea nchini humo hivyo wachezaji akiwemo Mpole kupewa nafasi ya kutafuta timu nyingine ili kulinda viwango vyao.

Mazungumzo baina ya Yanga na Mpole yanaendelea na kama watakubaliana kila kitu basi staa huyo wa Taifa Stars atakuwa Mwananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: