Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga imeizidi Simba mbali mno msimu huu - Mchambuzi

Yanga Rekodi Mpyaaaaa.jpeg Yanga imeizidi Simba mbali mno msimu huu - Mchambuzi

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya Soka katika Kituo cha EFM, Muwa Twalib amesema kuwa kwa soka wanalocheza Yanga Sc anawaona wakichukua ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu huu kwa mara ya tatu mfululizo.

Muwa Twalib amesema hayo mara baada ya kushuhudia michezo mitatu mfululizo Yanga ikifunga mabao matano kila mchezo jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye timu za Tanzania kwa miaka mingi.

"Kwa Yanga ambayo mimi nimeiona kwenye mechi hizi, kuna ziada ya ufanisi kwenye uwanja, ninaamini kwenye hilo. Kuna watu waliwahi kusema Simba bora inafungwa na Yanga dhaifu na Yanga bora inafungwa na Simba dhaifu, watu wajue kwamba tofauti ya ubora wa Simba na Yanga kwa msimu huu uwanjani msimu huu, Yanga wako mbali mno na haijawahi kutokea, ninaamini hivyo.

"Sijawahi kuona ubora wa Yanga mkubwa kwa kiasi hichi ambapo inaweza kukupa kila kitu uwanjani, wamejitosheleza kila idara, ninataka nije kuwapima kwenye mechi za kimataifa tena kwenye makundi sio hizi za awali sababu kwa Al-Merreikh unawaona Yanga wanapasua mapema na salama tu.

"Yanga wamesajili vizuri, wanacheza vizuri, kwenye Ligi ya ndani ukiangali ifike mahali watu wafahamu kwamba ukienda kucheza na Yanga uombe usifungwe tano lakini sio kuomba usifungwe kabisa, ufe lakini unakufa kifo gani? Watu waepuke kifo cha bao tano labda wabadilike tu kutoka kwenye hii form," amesema Muwa Twalib.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: