Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga hawakupaswa kubaki Avic Town - Jembe

Msigwa: Kila Kitu Kimekamilika Safari Ya Yanga Algeria Yanga hawakupaswa kubaki Avic Town - Jembe

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Saleh Ally 'Jembe' amesema kuwa Yanga walitakiwa kutoka na kwenda kuweka kambi nje ya Tanzania badala ya kuendelea kusalia nchini kwa miaka mitatu mfululizo.

Jembe ametoa kauli hiyo akisema pia kuwa kutoka kwao nje kungewasaidia kubadilisha mazingira na kuwaweka sawa kisaikolojia.

"Yanga wangeondoka Avic Town wakaenda kutafuta mazingira mengine lakini yawezekana wao wameona faida ya pale.

"Misimu miwili wamebaki Avic Town na wamefanikiwa kuchukua kila kitu japo walizidiwa vitu vichache kama idadi ya mabao ya kufungwa, mechi za kufungwa na mabao ya kufunga.

"Nashauri Yanga watoke kwa sababu wamekaa pale muda mwingi sana, hata Ulaya mfano Real Madrid wana kila kitu lakini wanalazimika kutoka nje ya Hispania na kwenda Marekani kuliko kuwa pale pale wachezaji wanalala vyumba vilevile.

"Kwa upande wa Simba watakuwa na deni kwa sababu walipewa kambi nje ya Tanzania na timu ikashika nafasi ya pili, hawakuondoka na kombe lolote," amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: