Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga ametoka Nabi amekuja Nabii - Oscar Oscar

Nabi Gamondi 2 WA0002 Yanga ametoka Nabi amekuja Nabii - Oscar Oscar

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mzee wa Kaliua Baba Mzungu mchambuzi wa masuala ya Soka katika Kituo cha Wasafi Media, Oscar George Oscar amesema kuwa Kocha mpya wa Yanga, Miguel Angel Gamondi ana uwezo mkubwa, tofauti na watu walivyokuwa wakimhofia baada ya kuondoka kwa Nasreddine Nabi.

Oscar amesema hayo mara baada ya kushuhudia michezo mitatu mfululizo Yanga ikifunga mabao matano kila mchezo jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye timu za Tanzania kwa miaka mingi.

"Yanga Sc walikuwa na Nabi wakashinda ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC back to back. Wakati anaondoka kocha Nabi ndani ya Yanga, kulikuwa na wasiwasi kwa baadhi ya mashabiki, lakini kwa mwanzo huu ni kama ametoka Nabi amekuja NABII, ngoja tusubiri muda tuone.

"Hakuna kitu kigumu kama kushinda mabao matano kwenye mchezo wa mpira wa miguu, hakuna mtu anaweza kukaa akachora huo mchoro wa namna ya kupata hayo mabao.

"Kufunga michezo miwili ya Ligi na mchezo mmoja wa Champions League mabao matano kila mechi, ni kiulizo, haiji kwa bahati mbaya na kuna namna inaogopesha ukiona timu ipo kwenye mtindo huo," amesema Oscar Oscar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: