Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tunazitaka pointi tatu za Mazembe

Yanga Kazini G Kikosi cha Yanga

Sat, 1 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa hauna maneno mengi zaidi ya kuhitaji pointi tatu za TP Mazembe kwenye mchezo wao wa mwisho wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi.

Kesho Aprili 2, Yanga watakuwa ugenini DR Congo kuwavaa Mazembe katika mchezo wa mwisho, ikumbukwe katika mchezo wao wa kwanza uliopigwa Dar, Yanga walishinda mabao 3-1.

Akizungumza nasi, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema kuwa, wanatambua ugumu wa mchezo huo lakini wamejiandaa kuhakikisha wanabeba alama tatu.

“Tuna mchezo dhidi ya TP Mazembe tunakumbuka tulipocheza nao hapa tulishinda na sasa tunawafuata tukiwa na ari ileile ya kusaka ushindi na kupata pointi tatu muhimu.

“Mashabiki tunatambua umuhimu wao na kuja kwao kutaongeza nguvu ndio maana tumewapa fursa ya kwenda kuiona timu yao ikitoa burudani na shangwe la kimataifa linahamia ugenini,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: