Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tunakwenda kuonesha ukubwa wetu Congo

Yanga Jeshi Kikosi cha Yanga wakifanya mazoezi

Sun, 2 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe unaotara¬jiwa kupigwa leo Aprili 2, mwaka huu, uongozi wa Yanga umet¬amba kuwa unataka kuutumia kuonesha ukubwa wa timu hiyo kwa kupata matokeo mazuri ugenini.

Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga tayari wame¬shakata tiketi ya kucheza robo fainali wakiwa wanaongoza msimamo wa Kundi D baada ya kufanikiwa kukusanya pointi 10 sawa na US Monas¬tir katika michezo yao mitano waliyocheza.

Akizungumza nasi, Mkuu wa Kitengo cha Habari za Mtandao Yanga, Priva Shayo ‘Privaldinho’ alisema: “Uzuri tunakwenda katika mchezo huu tukiwa na tiketi yetu ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo tuna kazi moja kubwa ya kwenda kuonesha ukubwa wa Yanga.

“Tunataka kuhakikisha tunapata matokeo mazuri na kuthibitisha kuwa kwa ukubwa wetu tunaweza kupata matokeo tukiwa popote pale.”

Jana Alhamisi, kikosi cha Yanga kilisafiri kutoka Dar hadi Lubumbashi nchini DR Congo, tayari kwa mchezo huo wa mwisho wa Kundi D.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: