Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tuna kisasi na Waarabu

Yanga Vs Bamako Mkapa Yanga

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, amechimba mkwara mzito kuwa sasa mawazo yao yote ni katika mchezo dhidi ya US Monastir ambao wanataka kulipiza kisasi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.

Mkwara huo umekuja baada ya Yanga kuifunga Real Bamako mabao 2-0, katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho Afrika Kundi D uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Ushindi huo umeifanya Yanga kufikisha pointi saba, ambapo kama wakiifunga US Monastir wikiendi ijayo, basi itafuzu robo fainali ya michuano hiyo kabla ya mchezo wa mwisho ugenini dhidi ya TP Mazembe.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya US Monastir uliochezwa nchini Tunisia, wenyeji waliibuka na ushindi wa mabao 2-0, hivyo Yanga wamepanga kulipa kisasi.

Akizungumza nasi, Kamwe alisema: “Baada ya kuibamiza Real Bamako, tumefanikiwa kufikisha pointi saba na ukiangalia msimamo wetu tunachotakiwa ni kupata ushindi mmoja tu, ili kufuzu robo fainali.

“Mchezo ujao ni dhidi ya US Monastir, kwetu huu mchezo umebeba mambo mawili makubwa, kwanza tunataka kuutumia kukata tiketi ya kucheza robo fainali, lakini tuna kazi kubwa na muhimu ya kulipa kisasi, kupitia mchezo huu lazima tuwaulize Monastir walitufungaje mabao mawili kwao.”

KUNDI D P W D L GF GA GD Pts 1. US Monastir 4 3 1 0 6 1 +5 10 2. Yanga 4 2 1 1 6 4 +2 7 3. TP Mazembe 4 1 0 3 4 7 −3 3 4. Real Bamako 4 0 2 2 3 7 −4 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: