Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tumewasoma Al-Merrikh, ushindi ni lazima!

Yanga Skudu Aucho Musonda.png Yanga: Tumewasoma Al-Merrikh, ushindi ni lazima!

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imesema kuwa imekwenda Kigali nchini Rwanda kwa lengo moja tu la kuondoka na ushindi dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan ili kazi iwe rahisi kwenye mchezo wa marudiano na si vinginevyo.

Hayo yamesemwa na Ofisa Mtendaji wa Yanga, Andre Mtine na kiungo wao Khalid Aucho mara baada ya kuwasili Kigali kwa ajili ya mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kupigwa kesho katita Dimba la Pele nchini humo.

“Tumejiandaa vizuri, tunaamini tutacheza vizuri na kushinda. Malengo yetu ni kucheza hatua ya makundi. Tumewasoma wapinzani wetu vizuri, mkiwa professional lazima muwasome wapinzani, benchi letu la ufundi limefanya hivyo,” amesema CEO Mtine.

Kwa upande wake, kiungo wa Yanga raia wa Uganda, Khalid Aucho amesema; “Sijawahi kucheza na Al-Merrikh, lakini tumewasoma kwenye video na namna ambavyo kocha anataka tucheze, kwa hiyo tutafanya kama ambavyo mwalimu atakataka ili kushinda mchezo huu.

Tumekuja hapa kushinda ili tukirudi Dar es Salaam, angalau kazi iwe nyepesi kwa upande wetu. Tusiposhinda hapa mchezo utakuwa mgumu Dar,” amesema Aucho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: