Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Tuko tayari kuwamaliza Waarabu

Yanga Geita Md Yanga: Tuko tayari kuwamaliza Waarabu

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir, uongozi wa Yanga kupitia kwa Ofisa Habari wao, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa tayari wamewasoma wapinzani wao na wamekamilisha asilimia zaidi ya 90 ya hesabu za maandalizi yao na kuchimba mkwara ni lazima wataibuka na ushindi.

Yanga ndio wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo wanatarajiwa kushuka uwanjani kesho Jumapili kuvaana na US Monastir katika mchezo wa tano wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika msimamo wa kundi D la mashindano hayo Yanga mpaka sasa wamefikisha pointi saba na kuendelea kushikilia nafasi ya pili ambapo sasa wanahitaji ushindi dhidi ya US Monastir ili kufuzu Robo fainali.

Akizungumza nasi, Kamwe alisema: “Tunaendelea na taratibu mbalimbali za hamasa kuelekea mchezo wetu dhidi ya US Monastir, mpaka sasa tumekamilisha zaidi ya asilimia 90 a maandalizi yetu tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tuna uhakika wa ushindi.

“Tumewasoma wapinzani wetu na tunajua ubora na mapungufu yao, hivyo licha ya kuutarajia mchezo mgumu lakini tuko tayari na tuna ari ya kuandika historia ya kucheza robo fainali baada ya muda mrefu kupita.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: