Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga, Simba zinarudi tena upya uwanjani

Simbaa Yanga Pic Siku 9 Yanga, Simba zinarudi tena upya uwanjani

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kufanya kweli na kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano ya kombe la shirikisho (ASFC), vigogo wa Soka nchini Simba na Yanga zinarejea tena kibaruani kusaka tiketi ya kutinga hatua inayofuata ya michuano hiyo mapema mwezi ujao.

Mbali na wababe hao wa soka nchini, Azam, Geita Gold, Ihefu, Mtibwa Sugar, Singida BS, Mbeya City, Prisons, Kagera Sugar na KMC kwa zitawakilisha upande wa ligi kuu, huku African Sports, Pan African, Green Warriors na JKT Tanzania zikiwakilisha Champioship.

Mapinduzi FC ndio timu pekee iliyofuzu kutoka ngazi ya Mkoa ikiwakilisha Mwanza kufuatia ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Polisi Katavi baada ya dakika 90 kuisha kwa suluhu.

Wekundu ndio watafungua pazia ya michuano hiyo ikiwaalika African Sports, mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam Machi 2, ilhali watani zao Yanga ambao ni bingwa mtetezi akimkaribisha Prisons Machi 3.

Geita Gold nao watakuwa uwanja wao wa Nyankumbu mjini Geita kuwapokea Green Warriors na siku inayofuata Ihefu itawavaa Pan African nyumbani, Mtibwa Sugar dhidi ya KMC na Singida BS ikiwavaa JKT Tanzania.

Hesabu ya kuwapata wababe nane itafungwa Machi 5 kwa timu za Azam kuwakaribisha Mapinduzi FC ilhali Kagera Sugar ikinyukana na Mbeya City, mechi ikipigwa uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Simba ilifuzu kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union, Yanga ikatakata 8-0 kwa Rhino Rangers, Azam akamnyoosha 4-1 Dodoma Jiji, Ihefu ikaitoa Namungo penalti 4-3, Singida BS wakafuzu kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting na JKT Tanzania ikaiondosha Polisi Tanzania kwa penalti 5-2.

Pan African wao walipata mteremko baada ya aliyekuwa mpinzani wake Gwambina FC kuingia mitini na baadaye kutangaza kujitoa kwenye soka, Green Warrios ikaichapa Mbuni 2-1 na African Sports wakaichakaza New Dundee penalti 4-2.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: