Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC ndiyo imembeba Nabi

Nabi Kocha Afrika Kocha Nabi.

Tue, 18 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka nchini kupitia TV3, Alex Ngereza amesema kuwa Klabu ya Yanga ndiyo imembeba aliyekuwa kocha wake, Nasreddine Nabi raia wa Tunisa.

Ngereza ametoa kauli hiyo baada ya Nabi kupata mafanikio makubwa akiwa na Yanga kisha kutimkia FAR Rabat ya Morocco ambako alitambulishwa jana kama kocha wao mkuu.

"Nabi sio kwamba alikuwa na kiwango kikubwa alipofika Yanga kilichomsaidia kufanya vizuri ni Yanga walisajili wachezaji wenye viwango vya hali ya juu.

"Nabi alipofika msimu wa kwanza hakufanya vizuri Yanga walimvumilia wakaenda kusajili wachezaji wazuri akapata kushindi ligi kwa hiyo hakuwa na kiwango cha kutisha ila wachezaji ambao walisajiliwa ndio ambao wamemsadia Nabi kufanya vizuri Yanga," amesema Alex Ngereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: