Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC: Malengo yetu hayajatimia

Yanga Vs Rivers United Yanga SC

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga umebainisha kuwa kazi bado haijaisha kwenye ligi na Kombe la Azam Sports Federation ili kukamilisha malengo waliyonayo ndani ya timu hiyo.

Yanga ni mabingwa watetezi wa ligi na Kombe la Azam Sports Federation, wanaongoza ligi wakiwa na pointi 68 huku wakiwa na kibarua cha kucheza nusu fainali ya Azam Sports dhidi ya Singida Big Stars.

Akizungumza nasi, Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa kila mipango ipo kwenye hesabu katika kufanikisha malengo yao.

“Kila mchezaji anatambua kuhusu malengo ambayo tupo nayo kwenye kutwaa mataji, tunahitaji kuona yale mataji ambayo tulitwaa msimu uliopita tunayabeba tena kwa wakati mwingine kwani bado kazi haijaisha tunarudi kivingine.

“Mashabaiki wazidi kuwa pamoja nasi unaona kwenye ligi bado kuna mechi zimebaki ambazo hizi ni muhimu kwetu kupata matokeo na kwenye Kombe la Azam Sports pia tunakwenda kupambana kupata matokeo mazuri,” alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: