Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga SC: Geita kapita sasa bado Kagera, Simba SC

Mayele Simuuu Mayele

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports, benchi la ufundi la Yanga limechimba mkwara mzito kuwa sasa wanataka pointi sita za michezo yao miwili ijayo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar na Simba.

Yanga juzi Jumamosi walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa robo fainali ya ASFC uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam na kufanikiwa kutinga nusu fainali ya mashindano hayo wanayoyatetea.

Kesho Jumanne Yanga wanatarajiwa kuvaana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex na mara baada ya mchezo huo wanatarajiwa kuvaana na Simba katika mchezo wa Kariakoo Dabi ambao umepangwa kupigwa Aprili 16, mwaka huu.

Akizungumza nasi, Meneja wa Yanga, Walter Harrison alisema: “Tunashukuru kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya ASFC kupitia ushindi wetu dhidi ya Geita Gold, kwa sasa hakuna muda wa kupumzika kwani tuna ratiba ya michezo miwili muhimu ya Ligi Kuu Bara.

“Tuna mchezo dhidi ya Kagera Sugar Jumanne na mchezo dhidi ya Simba Aprili 16, malengo yetu ni kushinda mechi hizo na kujiweka karibu zaidi kutetea ubingwa wetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: