Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Princes vs Simba Queens hakuna mbabe

Simba Yanga Queens Yanga Princes vs Simba Queens

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (Serengeti Lite Women’s Premier League #SLWPL) kati ya Yanga Princes na Simba Queens umemalizika katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam kwa timu hizo kutoshana nguvu baada ya kutoa sare ya bao 1-1.

Katika mchezo huo ambao Yanga Princes walikuwa wenyeji, Simba Queens ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kuinako dakika ya 30 kupitia kwa Jentrix Shikangwa dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza, bao lililodumu mpaka kipindi cha pili kabla ya Yanga kusawadhisha dakika ya 75 kupitia kwa Wogu Chioma.

Kwa matokeo hayo, Simba wakiwa na alama 27 wameshuka kutoka nafasi ya kwanza mpaka ya tatu kufuatia ushindi wa Foutain Gate dhidi ya Mkwawa ambapo Fountain wamepanda mpaka nafasi ya kwanza wakifikisha alama 29, na ya pili ikishikwa na JKT wenye alama 28.

Matokeo mengine;

Baobab 0-3 JKT

Mkwawa 0-2 Foutain Gate

Wafungaji;

Priviledge Mupeti

Neema Paul

Msimamo wa Ligi;

Fountain Gate - 29

JKT - 28

Simba Queens - 27

Yanga Princes - 22.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: