Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Mtachagua wenyewe tuwafunge ngapi

Kamwe Tena Ms.jpeg Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

uongozi wa Yanga, umebainisha kuwa, wapinzani watachagua mabao mangapi wafungwe watakapokutana kuanzia msimu wa 2023/24 kutokana na ubora walionao.

Ni Avic Town, Kigamboni, Dar, hapo ipo kambi ya Yanga wakiwa ni mabingwa watetezi wa Ngao ya Jamii, Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports, mataji waliyobeba msimu wa 2022/23.

Akizungumza nasi, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Kwa namna ambavyo wachezaji wanajituma na wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya, tutakuwa tunachagua wapinzani wetu tuwafunge mabao mangapi.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye kila wakati kwa kuwa wao sehemu ya mafanikio yetu unaona msimu wa 2022/23 tumefanya vizuri tunahitaji kuendelea kuwa bora zaidi.

“Msimu huu mpya tunakwenda kufanya kazi bora zaidi kwani kila mchezaji yupo tayari na benchi la ufundi pia linapenda kuona matokeo uwanjani tuzidi kuwa pamoja.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: