Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Jumamosi ni 'Maxi Day'

Maxi Nzengeli Kikosini Maxi Nzengeli.

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga wameipa jina la 'Max Day' mchezo wa marudiano wa kimataifa dhidi ya ASAS Ya Djibouti na kuuita jina hilo.

Mchezo huo utakaochezwa Azam Complex Chamazi umeitwa jina la kiungo huyo mshambuliaji kutoka nchini Congo, Max Nzengeli.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisa Habari wa timu hiyo @alikamwe amesema wameamua kuuita jina hilo kutokana na mchango wa kiungo huyo.

Kamwe aliwataka mashabiki waje kiwanjani siku hiyo wakiwa wamevaa kwa kuchomokea kama anavyovaa kiungo huyo.

“Huu mchezo wetu wa Jumamosi tumeupa jina la Max Day na tunawataka mashabiki waje kiwanjani wakiwa wamechomekea nguo zao,” alisema Kamwe

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: