Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga: Hatumwachii Mayele

Mayele Yanga 170x650 Fiston Mayele

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga upo Katika mazungumzo na mshambuliaji Fiston kalala Mayele kwa ajili ya kumwongeza mkataba mpya ambao utamfanya asalie kwenye kikosi cha Yanga.

Awali mkataba wa Fiston kalala Mayele ulikuwa umebaki mwaka mmoja baada ya kusaini mkataba mpya mwanzoni mwa msimu huu 2022-2023.

Yanga wamepanga kumpa mkataba wa miaka miwili Fiston kalala Mayele na kumfanya kuwa mchezaji ambaye analipwa pesa nyingi Tanzania.

Hadi sasa bado mazungumzo yanaendelea baina na Menejimenti ya mshambuliaji Fiston kalala Mayele na Uongozi wa Yanga.

Fiston kalala Mayele amewapa nafasi kubwa Yanga kutaka kuendelea kusalia kwenye kikosi cha mabingwa wa Nbc,,Asfc, Fiston kalala Mayele bado ana mapenzi na Yanga na hana wasiwasi na Uongozi wake Yanga juu ya kumpatia mkataba mpya.Licha ya kupata ofa nyingi Kutoka nje ya Tanzania.

Fiston kalala Mayele ambaye kwa sasa yupo nchini Tanzania pamoja na familia yake akiendelea na likizo ambayo Uongozi umewapatia wachezaji wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: