Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Yanga Bingwa tena msimu huu - Muwa Twalib

Gamondi X Yanga Somo Yanga Bingwa tena msimu huu - Muwa Twalib

Thu, 31 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya Soka katika Kituo cha EFM, Muwa Twalib amesema kuwa kwa soka wanalocheza Yanga Sc anawaona wakichukua ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC kwa msimu huu kwa mara ya tatu mfululizo.

Muwa Twalib amesema hayo mara baada ya kushuhudia michezo mitatu mfululizo Yanga ikifunga mabao matano kila mchezo jambo ambalo halijawahi kutokea kwenye timu za Tanzania kwa miaka mingi.

"Nimeandika mimi kwamba wa kushiba unaonekana kwenye sinia, na nimeshawahi kusema kwamba Yanga Bingwa msimu huu. Wakati Yanga wanamaliza mechi yao ya CAFCL dhidi ya ASA FC ya Djibouti niliandika kuwa Yanga Bora…, Yanga Bora…, Yanga Bora…, Yanga Bora…, Yanga Bora…. sikuandika kawaida kwa sababu inafika hatua ukiandika uchambuzi wa Yanga unaonekana kama mnafiki.

"Yanga wanatuchanganya, wakati tunamuimba Pacome anakuja Max anaua. Yanga hii mchezaji anayefanya balaa mechi hii, kwenye mechi ijayo akikaa jukwaani akacheza mwingine wala hukumbuki kama kuna mtu amefanya balaa mchezo uliopita, ni timu ambayo ina madhara makubwa sana uwanjani.

"Nimeshasema kwamba yanga Bingwa lakini ubingwa ninaowapa Yanga kama wataendelea hivi, kushinda na kupata mabao mengi kila mchezo, kuamini kwamba wao ni wakubwa wanapaswa kuua tu, hili jambo litawafikisha pazuri sababu wana timu bora sana," amesema Muwa Twalib.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: