Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wenye nchi wameitika mapema tu

Mashabiki Simba Kwa Mkapa.jpeg Wenye nchi wameitika mapema tu

Sun, 6 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ikiwa ni saa tano tu zimepita tangu kufunguliwa kwa mageti ya Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo leo, Jumapili Simba wanajambo lao tayari kumetapika.

Huenda muda mchache ujao Simba ikatangaza kuujaza Uwanja huu mbapo wanafanya tamasha lao la 15 ikiwa ni maalumu kwa ajili ya kufanya utambulisho wa wachezaji na benchi lao la ufundi kwa ajili ya msimu ujao wa 2023/24.

Ikumbukwe kuwa Simba ilitangaza kumaliza tiketi za tamasha hili siku tatu kabla na kuweka rekodi.

Burudani mbalimbali zinaendele Uwanja hapa huku mashabiki wakipiga stori za hap na pale kuhusu chama lao kuelekea msimu ujao.

Wafanyabiashara ndogondogo kama vile matunda, maji na juisi nao wanendelea na yao.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: