Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waziri Ndumbaro, Karia watua kambini Yanga

Ndumbaro X Aziz KI Waziri Ndumbaro, Karia watua kambini Yanga

Fri, 29 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro amefanya ziara fupi kwenye kambi ya Yanga inayojiandaa kumalizana na Al Merreikh ya Sudan kesho.

Ndumbaro amefanya ziara hiyo akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallece Karia aliyeambatana na makamu wake Athuman Nyamlani kisha wakateta na kikosi hicho.

Ndumbaro amewataka wachezaji wa Yanga kuhakikisha wanafanya kweli kwenye mchezo wa marudiano wa kesho utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex wakiwania tiketi ya kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Sisi kama Serikali tunawaona ninyi kama mabalozi wa Tanzania mnakwenda kuwawakilisha nchi mnabeba thamana kubwa ya Watanzania milioni sitini na mbili,"amesema Ndumbaro.

Kwa upande wake Rais Karia mbali na kuwapongeza Yanga kwa ushindi mzuri wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini amewataka kumalizia mechi ya kesho vizuri watakapocheza nyumbani.

"Mtaingia kwenye mchezo wa kesho bila msongo wa mawazo mnachotakiwa kufanya kesho ni kumalizia kazi ingawa hautakuwa mchezo rahisi sisi kama viongozi jukumu letu kama kawaida tumekuja hapa kuwapa nguvu."

Mapema Rais wa Yanga injinia Hersi Said ambaye ameambatana na makamu wake Arafat Haji na wajumbe wa kamati ya mashindano ameishukuru serikali na TFF kwa kufika mazoezini kwao huku akiwapongeza pia kwa hatua ya kufanikisha Tanzania kuwa muongoni mwa nchi tatu zitakazoandaa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2027.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: