Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washambuliaji waanza na moto Ligi Kuu

Baleke Onana Washambuliaji waanza na moto Ligi Kuu

Thu, 24 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji wameonekana kuanza vyema katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu kutokana na kasi ya kufumania nyavu waliyoionyesha katika raundi mbili za mwanzo kulinganisha na nyota wa nafasi nyingine.

Kabla ya mchezo wa juzi baina ya Singida Big Stars na Tanzania Prisons, idadi kubwa ya mabao ilikuwa imepachikwa na washambuliaji huku viungo wakifuatia, wakati huo mabeki wakionekana kutoka patupu.

Hadi kufikia juzi idadi ya mabao 23 ilikuwa imefungwa katika mechi 11 za ligi hiyo ambapo kati ya hayo, mabao 15 yakiwa yamefungwa na wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji, mabao saba yakiwa yamepachikwa na viungo na moja likiwa la kujifunga la kipa.

Washambuliaji walioanza vyema vita ya kuwania kiatu cha ufungaji bora msimu huu ni Jean Baleke wa Simba na Mateo Anthony wa Mtibwa Sugar ambao kila mmoja amefumania nyavu mara mbili katika mechi mbili za mwanzo za timu zao.

Wakati Anthony akifunga mabao yake mawili katika mechi dhidi ya Simba, Baleke yeye alipachika moja pindi walipocheza na Mtibwa Sugar na lingine akafunga dhidi ya Dodoma Jiji.

Ukiondoa hao, wengine ambao wamefunga bao mojamoja ni Moses Phiri na Willy Onana (Simba), Adam Adam na Othman Dunia (Mashujaa), Prince Dube (Azam), Elias Maguli (Geita Gold), Hija Ugando (Coastal Union), Kassim Tiote (Mtibwa Sugar), Martin Kiggi (JKT Tanzania), Fabrice Ngoyi (Namungo), Moubarack Hamza (Ihefu) na Rashid Chambo (KMC).

Viungo waliopachika mabao saba ni Feisal Salum wa Azam FC ambaye amefumania nyavu mara tatu na hivyo anaongoza chati ya ufungaji bora, Clatous Chama na Fabrice wa Simba ambao kila mmoja amefunga bao moja kama ilivyo kwa Ibarhim Ajibu (Coastal Union) na Meshack Mwamita (Dodoma Jiji).

Goli lingine moja ni la kujifunga la kipa wa Coasta Union, Justin Ndikumana.

Kocha wa Mashujaa FC, Mohamed Abdallah 'Baresi' alisema kuwa bado ni mapema kutabiri nani atafanya vizuri kwenye ufungaji kwa vile ligi ndio imeanza.

"Wameanza vizuri lakini changamoto kubwa ni muendelezo. Wale watakaokuwa na muendelezo mzuri watakuwa na nafasi kubwa ya kumaliza vizuri hivyo ni suala la kusubiri na kuona," alisema Baresi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: