Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wanasema "Sisi ndiyo Yangaaa!"

Yangaaaaa Gsh Wananchi wanasema

Mon, 1 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya kubanwa mbavu na kuambulia suluhu mbele ya wapinzani wao jana Jumapili lakini jambo hilo halikuweza kuwazuia Yanga kuweza kuweka rekodi yao ya kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga jana Jumapili wakiwa kwenye Dimba la Mkapa, Dar walijikuta wakikumbana na upinzani wa juu kutoka kwa wapinzani wao hao ambapo ushindi wa mabao 2-0 walioupata kwenye mchezo wa kwanza nchini Nigeria uliweza kuwabeba na kufanikiwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Kwenye mchezo huo Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa ya nyota wake akiwatumia baadhi ya wachezaji ambao hawakuwa wanaanza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza kutokana na matokeo ya mechi ya kwanza kuwabeba.

Katika mchezo huo mastraika wa Yanga licha ya kufanya majaribio kadhaa lakini walikuta mambo magumu baada ya kipa wa Rivers kuwa kikwazo kwa nyavu zake kutunguliwa.

Straika wa Yanga, Clement Mzize alianza kwenye kikosi cha kwanza na alifanya majaribio ambayo hayakulenga lango ilikuwa dakika ya 12, 22.

Mzee wa kutetema, Fiston Mayele jaribio lake la dakika ya 16 lililenga lango ila liliokolewa na kipa wa Rivers United.

Shukran kwa mdaka mishale, Djigui Diarra ambaye alifanya kazi yake kwa umakini kutimiza majukumu yake na aliokoa hatari dakika ya 4, 10, 15, 16, 20, 26, 29, 32.

Kwenye mchezo huo dakika ya 25, mchezo ulisimama kwa muda kutokana na hitilafu ya umeme kabla mambo kukaa sawa ambapo mchezo uliendelea.

Kwenye hatua ya nusu fainali Yanga wanakwenda kukutana na Marumo Gallants ya Afrika Kusini ambayo ilishinda kwa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Pyramids yaa Misri, kwa kuwa robo fainali ya kwanza walitoshana nguvu wa kufungana bao 1-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: