Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi mmemsikia Kocha Gamondi?

Gamondi 00 Kocha Gamondi.

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Klabu ya Yanga, Miguel Angel Gamondi amesema kuwa angetamani kushinda kama ilivyo kwa Kaizer Chiefs lakini mchezo wa leo ni wa Pre-season anaweza kushinda ama kupoteza kikubwa ni kuwapa wachezaji nafasi ya kuonesha uwezo wao.

Kocha huyo amesema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari na kuongeza kuwa hatofanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi kwakuwa kilikuwa bora msimu uliyopita hivyo hakuna haja ya kufanya hivyo.

Mchezo huo wa kirafiki wa Yanga Sc dhidi ya Kaizer utapigwa leo saa 1:00 jioni katika Dimba la Mkapa ikiwa ni kuchagiza sherehe za kilele cha Wiki ya Mwananchi ambazo zitaendana na utambulisho wa wachezaji wapya wa Yanga.

Kocha Miguel alisema “Kesho (leo) ni siku kubwa kwa Mashabiki wa Young Africans SC pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania Klabu hii kubwa yenye historia kubwa.

“Kwenye upande wa timu bado tuko kwenye maandalizi, na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs  tutautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yetu kwa msimu ujao.

Huku akidokezea mipango yake ya msimu ujao, “Tunatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwasababu hii ni Klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka Klabu hii iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: