Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanajeshi wa Nabi waingia chimbo

Yanga Kazini G Mastaa wa Yanga wakipiga tizi.

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Kocha Mkuu wa Yanga Mtunisia, Nasreddine Nabi juzi liliingia kambini tayari kwa mchezo wa mwisho wa makundi wa Kombe la Shirkisho Afrika huku likianza na program ya fiziki pekee.

Yanga katika mchezo huo, watacheza dhidi ya TP Mazembe Aprili 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa TP Mazembe, Lubumbashi nchini DR Congo saa 10:00 Jioni.

Katika mchezo huo, Yanga wataingia uwanjani kwa ajili ya kukamilisha ratiba pekee, kwani tayari wameshafuzu katika Kundi, D huku TP Mazembe wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1.

Akizungumza nasi, Nabi alisema kuwa mchezo huo wanauchukulia umuhimu mkubwa, kwani wanazihitaji pointi za TP Mazembe ili wabakie kileleni katika msimamo ambao wana pointi 10 sawa na US Monastir waliofuzu hatua ya robo fainali.

Nabi alisema kuwa, kikosi chao kimeingia kambini juzi Jumatatu kikiwa chini ya kocha msaidizi Mrundi Cedric Kaze kwa kuanzana program ya fitinesi pekee kukimbia mbio fupi na ndefu kwa ajili ya kurejesha utimamu wa mwili wachezaji wao.

Aliongeza kuwa program hiyo iliwahusisha wachezaji waliobakia kambini wakiendelea na mazoezi huku wakiwasubiria wengine waliookuwepo katika majukumu ya timu za taifa.

“Nimewataka wachezaji wangu wote waingie kambini, ruhusa ikiwa kwa wachezai wale ambao wapo katika majukumu ya timu za taifa pekee na majeruhi.

“Lakini wote waliobakia wanatakiwa kuingia kambini, nashukuru katika hilo limefanikiwa hakuna mchezaji yeyote aliyekosekana kambini na wote wameripoti tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya TP Mazembe.

“Wachezaji hao wameanza na program ya mazoezi ya fitinesi baada ya wachezaji kutoka katika mapumziko ambayo tulipawa mara baada ya mchezo dhidi ya US Monastir,” alisema Nabi.

MATOKEO YA YANGA CAF Monastir 2-0 Yanga Yanga 3-1 Mazembe Bamako 1-1 Yanga Yanga 2-0 Bamako Yanga 2-0 Monastir.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: