Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakili Patrick Simon: Kijana Mahakama sio mama yako

SIMON FEI TOTO Wakili Patrick Simon

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imemtaka mchezaji wao, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kuacha ujeuri na kuitunishia misuli klabu yake hiyo badala yake afuate taratibu ikiwemo kwenda klabuni hapo na kufanya makubaliano na uongozi ili aweze kuondoka kwa heri.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Sheria wa Klabu ya Yanga, Wakili Patrick Simon mara baada ya kesi hiyo kushindwa kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF kufuatia klabu hiyo kupelekea mapingamizi baada ya Fei Toto kuomba kuvunja mkataba wake na Yanga.

"Bwana mdogo hakufukuzwa Yanga, kukaa nje anajitakia mwenyewe. Klabu ishatoa msimamo wake toka tarehe 6/3/2023; Kijana akitaka kurudi anakaribishwa, akitaka kuondoka aje tubariki safari yake, kama kuna timu inamtaka ije mezani.

"TFF na Kamati zinapotezewa muda, mkataba baina ya Yanga na Kijana hauwezi kuvunjwa na mtu yoyote tofauti na wahusika wa mkataba tu, na Yanga haijapokea maombi ya kuvunja mkataba.

"Kama mtu akiandika barua kirahisi vile na akatokomea kusikojulikana badae akaibuka kutaka kamati ibariki utoro wake kazini, unakua umeweka precedent mbaya sana ambayo kuna siku utaamka asubuhi ukute timu flani wachezaji wake wote wamechukuliwa kwa style ya kuandika tu barua na kusababisha ligi kushindwa kuendelea.

"Kwa wanaomuonea huruma eti kijana kiwango chake kitapotea, nawakumbusha kwamba Kijana hajafukuzwa, aliamua kutoroka kambini na kuchagua kwenda kufanya mazoezi mwenyewe kwenye fukwe za Zanzibar.

"Haki hutendeka kwa kufata sheria sio kwa kutafuta huruma. Nawaomba WanaYanga tuendelee na maandalizi ya mechi yetu ya derby, hii ni mechi muhimu sana kwetu, haya mengine yasiwapotezee muda.

"NB: Kuna msemo wa kisheria husema “The Court is not your mother to give you whatever you want“ - yaani /Mahakama sio mama yako kukupa kila ukitakacho/."

Fei Toto jana Aprili 12 alifika mbele ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji kujua hatma ya barua yake ya kuomba kuvunja mkataba na klabu ya Yanga.

Fei Toto aliongozana na wakili wake Fatma Karume ambaye baada ya kumaliza kusikilizwa leo amesema kuna vitu vya kisheria vinatakiwa kuwasilishwa Aprili 18 na 25 na Mei 4 ndipo rasmi shauri litasikilizwa tena.

Sehemu ya barua inayotajwa kuandikwa na Feisal Salum kwenda TFF akihitaji kuvunja mkataba na Yanga. Amesema amepitia manyanyaso Jangwani na anaomba akacheze kule anapothaminiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: