Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wakali wa pasi ndefu Yanga waingia kwenye vita kubwa

Mkude Sure0049 Wakali wa pasi ndefu Yanga waingia kwenye vita kubwa

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakali wa pasi ndefu ndani ya Yanga na Simba, leo wanatarajiwa kuwa kwenye vita nyingine ya kumsaka mbabe atakayetoka na tabasamu baada ya dakika 90.

Ni kwenye mchezo wa kumsaka mshindi wa Ngao ya Jamii inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Yanga miongoni mwa wakali kwenye pasi ndefu ni kipa namba moja, Djigui Diarra ambaye katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam FC, alifanya yake kwa kupiga pasi ndefu zaidi ya 7, mwingine ni Yao Attohoula aliyepiga pasi ndefu zaidi ya sita.

Simba nao sio kinyonge, kipa wao namba mbili, Ally Salim hana mambo mengi kwa upande wa pasi ndefu, ila Henock Inonga yeye ni mtaalamu wa pasi ndefu. Katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida Fountain Gate, alipiga pasi ndefu dakika ya 28, 45, 60, 63, 66. Mwingine ni kiungo wa kazi ngumu Mzamiru Yassin, huyu alipiga pasi ndefu dakika ya 31, 34 na 36.

Kazi kubwa inatarajiwa kuwa leo kwa mastaa hao ikiwa watapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza ama kutokea benchi kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: