Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau wafunguka kuzisaidia Simba, Yanga na Singida FG kimataifa

Yanga X Simba Balaa Wadau wafunguka kuzisaidia Simba, Yanga na Singida FG kimataifa

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Wawakilishi wa Tanzania Kimataifa Simba, Yanga na Singida Big Stars kwenda raundi ya pili Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika, wadau wa soka wamejitokeza na kueleza nini kifanyike kwa timu zetu zifanye vizuri Kimataifa.

Kwenye mdahalo wa X Space unaoendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), wadau walichangia kuhusu nini kifanyike kwa klabu za Tanzania zifanye vizuri Kimataifa.

Akizungumza hilo Nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Mohamed Hussein 'Mmachinga' amesema anaamini Jambo litakaloweza kuzifanya timu zetu kufanya vizuri kimataifa ni ubora wa wachezaji ambao wataisaidia.

"Timu zetu zimepiga hatua kubwa kutokana na ubora wa wachezaji hususani wale wa kigeni hivyo ukichanganya na waliopo naamini tutafanya vizuri," amesema na kuongeza

"Yanga nimefurahi inavyocheza kwa sababu ukiangalia msimu uliopita ilikuwa inategemea mchezaji mmoja ila msimu huu kila mmoja anaweza kukufunga japo wanatakiwa wawe makini kwenye eneo la katikati na Simba inapaswa kuongeza umakini zaidi kwenye eneo la ushambuliaji tofauti na maeneo mengine japo hayo ni maoni yangu tu" Mohamed Hussein 'Mmachinga'

Kwa upande Beki wa zamani wa Simba na Yanga, Amir Maftah amesema ili klabu za Tanzania zifanye vizuri kwenye michuano ya kimataifa (CAF), wachezaji wanatakiwa kuongeza umakini kuzingatia wanayoambiwa na makocha wao.

"Simba, Yanga na Azam FC ukiondoa Singida Big Stars, zina uzoefu, naamini zinaweza zikafika mbali zaidi, zikijipanga na kujua wanakwama wapi kwa muda mwingi walioshiriki huko nyuma" aamesema na kuongeza;

"Ingawa kwa Simba bado hawana na kombinesheni nzuri kama ila siyo sababu ya kushindwa kufanya vizuri, timu zote hazitakiwa kudharau wapinzani wao," amesema Maftah na kuongeza;

Akichangia mjadala huu mchezaji wa zamani wa Yanga, William Mtendamema amesema ili timu za Tanzania zifanye vizuri Kimataifa zinahitaji usajili bora utakaowasaidia na sio kuleta wimbi kubwa la wachezaji kutoka nje.

"Kumekuwa na wimbi kubwa la wachezaji kutoka nje na wengine wameonyesha thamani yao japo wengine bado, mbali na mastaa bora ila hata suala la viongozi tunahitaji wenye maono na soka," amesema

"Simba na Yanga zimejitahidi sana kwenye usajili wao msimu huu japo kwa Singida Big Stars licha ya kuchipukia ila nao sio mbaya sana," amesema na kuongeza "Nashauri wachezaji wa timu zote kujitambua kwamba wako kwenye mashindano gani na hilo ni jukumu la kocha kwa sababu michezo ya ligi na ya kimataifa ni tofauti japo wanatakiwa kujua wanahitaji nini," amesema William Mtendamema

Aidha mchezaji wa zamani, Oscar Joshua amesema usajili bora ndio siri ya timu za Tanzania kufanya vizuri kimataifa huku akiwataka viongozi wa klabu hizo kila mmoja kutimiza majukumu yake.

"Wawekeze kwenye mpira kwa sababu tunaona wachezaji wanasajiliwa kwa Sh1 bilioni hadi na zaidi sasa kama Tanzania tunataka kupiga hatua kama hiyo ni lazima tuwekeze na tuache ujanja ujanja,"

"Tanzania sisi ni waoga ndio maana hatuwezi kufanya vizuri na utaona Madagascar, Comorro na mataifa mengine tuliowazidi wanatufunga huko mbeleni kwa sababu wenzetu wanabadilika,"-mchezaji wa zamani, Oscar Joshua

Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi, Devotha Kihwelo amemalizia nakusemaa ili timu za Tanzania zifanye vizuri Kimataifa ni lazima viongozi wawaache makocha wafanye kile wanachoamini wataweza kuisaidia timu kufikia malengo.

"Kwanza timu zipewe nafasi kwa maana ya kocha kusajili wachezaji anaoona wanafaa ili waweze kufanya vizuri, tumeona hivi karibuni kocha ameachia ngazi kwa sababu ya kuona kile alichokitarajia sicho alichokipata," amesema Devotha

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: