Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachezaji wengi Afrika wanasaini tu sababu wanaona pesa nyingi - Jasmine

Fei Yanga Fd.jpeg Wachezaji wengi Afrika wanasaini tu sababu wanaona pesa nyingi - Jasmine

Sun, 16 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimamizi wa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum 'Fei Toto', Jasmine Razack amesema kuwa kwa uzoefu wake amekutana na kesi nyingi za wachezaji kuingia kwenye migogoro na timu zao kwa sababu mbalimbali.

Jasmine amesema kuwa, wachezaji wengi wa Afrika wamekuwa wakisaini mikata yao na vilabu bila kujua kilichomo ndani ya mikataba hiyo huku wakikimbilia pesa walizoqhidiwa ama kupewa pasi na uelewa wa changamoto wanazoweza kukutana nazo kutokana na mikataba hiyo.

“Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwasimamia wachezaji wa nje, kwa mfano Emanuel Ebue aliwahi kupitia kwenye changamoto za kimikataba. Akiwa Ulaya kuna wakati alikwaruzana na msimamizi wake wakashindwana, wakati tunahangaika na kesi yake nikamuuliza kwa nini alisaini mkataba wa aina ile?

“Akaniambia, wazazi wake walifariki na yeye alilelewa na bibi yake ambaye alikuwa anauza tumbaku sokoni kupata fedha ya kujikimu. Alipokuja mtu kuniambia ananipeleka Ulaya ninaweza kupata hadi dola 10,000 kama mchezaji unafikiri nawaza nin?

“Ebue anasema alipoletewa mkataba akasaini chapchap na kutia dole gumba! Kwa hiyo ni vigumu kuwalaumu hawa wachezaji kwa sababu wakati mwingine wanafanya hivyo kwa sababu ya hali zao na familia zao.”

“Kwa hiyo sisi ambao tunafahamu pamoja na hizi klabu zetu tunapaswa kuwasaidia wachezaji wa aina hii. Ulaya matatizo ya aina hii yalikuwa mengi hadi wakatunga sheria kwa hiyo klabu zinaogopa kuwasainisha mikataba tu kiholela,” amesema Jasmine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: