Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wachambuzi wapishana usajili wa Mkude Yanga

Mkude Yanga 8040736 Wachambuzi wapishana usajili wa Mkude Yanga

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya soka nchini wamepishana kimtazama kuhusu usajili walioufanya Yanga SC wa kiungo mkabaji Jonas Mkude kutoka kwa watani zao SImba Sc.

Mchambuzi wa Wasafi FM, Hans Raphael

"Usajili wa Jonas Mkude kwenda yanga ni usajili wa KUKOMOANA. Tatizo la Yanga ni wingers, hawajatibu tatizo la winger wanasajili kiungo. Ni usajili wa kukomoa tu."

Mchambuzi wa Channel Ten, Juma Ayo

"Kwa ushindani wa humuhumu ndani ni usajili mzuri sana lakini kwa usajili wa kushindana na USM Alger kimataifa aisee ni ngumu kutoboa. Yanga wamemsaidia Mkude kuliko ambavyo Mkude ataisaidia Yanga."

Mchambuzi wa EFM, Wilson Oruma Mzee wa Jambia'

"Yanga wamemchukua Mkude kupindi ameshachoka, ukikaa sana sehemu moja unazoeleka, Yanga wanakwenda kumpa nafasi ya kurejea kwenye ubora wake, huniambii kocha Gamondi anamfahamu Mkude, huu ni usajili wa mapendekezo ya viongozi"

Mwandishi; Sospeter Ilagila.

Nitakuwa tofauti kidogo na baadhi ya wachambuzi walionukuliwa wakisema, usajili wa Mkude.

◉ Kwanza kabisa tukumbuke kuwa msimu una mashindano mengi.

-Ligi kuu Tanzania bara

-Champions league

-FA Cup etc.

◉ Kwa hiyo rotation na idadi ya namba ya wachezaji bora kikosini inatakiwa iwe kubwa. Hapa nazungumzia wale wa kimataifa / wa kigeni na wazawa / Wa-Tanzania.

◉ Mkude ni mzawa, na hakuna asiyejua uwezo wake. Kwa wazawa ni addition nzuri, class ya Mkude huwezi kuipata kirahisi kutoka katika vilabu vingine (Kwa wazawa).

◉ Ingekuwa Jonas Mkude ni mchezaji wa Nje ya Nchi wangekuwa na hoja kwa sababu angeenda kuongeza namba ya Wachezaji wa kigeni ambao wana (12).

◉ Kusema Yanga bado haijatibu tatizo hususani kuhusu Wingers ni kuukosea uongozi wa Yanga. Sidhani kama wamesema kuwa Jonas Mkude ni moja kati ya viungo bora sana wazawa kwenye eneo analocheza.

Kudumu timu kubwa kama Simba kwa misimu zaidi ya 10 sio bahati mbaya na haitokei mara nyingi hasa kwa vilabu vyetu visivyo na roho ya uvumilivu.

Kama haitokei mara nyingi basi ujue inapotokea ujue kuna sababu ya tofauti ambayo siku zote ni QUALITY.

Yes, kwenye football hakuna radha isiyochosha kama uwezo wa kuisaidia timu majukumu kwa ufanisi. Bahati mbaya kwa Jonas alipitia kipindi kigumu kidogo kilichokuwa na changamoto ya nje ya uwanja.

Yanga wamepata Mtu...Yanga wamepata kiungo CHUMA! Kama akiwa fiti kwa asilimia 80 tu hakuna kiungo wa kumuweka benchi pale Yanga.

Bahati nzuri kwa Yanga wana nyota na wachezaji wa aina hii... Mudathir Yahaya amethibitisha hilo hivi karibuni. Kila la heri Mwamba @jonasmkude20."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: