Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vibe la Yanga lahamia Congo

YANGA MASHABIKI ER.jpeg Vibe la Yanga lahamia Congo

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutinga hatua ya robo fainali Yanga imeanza hesabu za mchezo wao ujao wa kimataifa dhidi ya TP Mazembe.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 2 DR Congo. Ikumbukwe kwamba mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Yanga 3-1 TP Mazembe.

Kwenye mchezo huo ni Kennedy Musonda, Mudhathir Yahya na Tuisila Kisinda ambaye alianzia benchi walipeleka maumivu kwa wapinzani wao.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa sasa wanapeleka shangwe DR Congo. “Wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Yanga sasa tunapeleka shangwe la Kimataifa ugenini twende Congo kwa Tsh 700,000 tu! (Full Package),”.

"Tunajivunia kuwa na mashabiki bora kwenye Klabu na hili tumelidhibitisha kwenye michezo yetu mitatu ya Kimataifa tukiwa nyumbani na sasa Uongozi wa Klabu umeamua lazima usafiri na mashabiki wake kwenda nao Congo kwenye mchezo wetu wa mwisho kwenye hatua ya makundi"

"Tuna idadi kubwa ya wachezaji walioitwa kwenye timu zao za taifa, wachezaji ambao wapo watarudi rasmi mazoezini kesho tayari kwa maandalizi ya mchezo wetu ujao na wa mwisho kwenye hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe na kambi rasmi ya mazoezi itaaanza tarehe 27."

Yanga imetoa gari kwa ajili ya safari kuelekea DR Congo kwa mashabiki kupata fursa ya kuhushudia mchezo huo ambapo watato tiketi bure kwa mashabiki watakaokuwa kwenye safari hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: