Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VAR kuhusika Rivers United vs Yanga

Yanga Tizi Geita Yanga wakipasha misuli

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tayari wawakilishi wa Tanzania kwenye anga za kimataifa Yanga katika Kombe la Shirikisho Afrika wameanza safari kuibukia nchini Nigeria.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Rivers United ya Nigeria ambao ni hatua ya robo fainali.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 23, 2023 ambapo mchezo huo baina ya Rivers United vs Yanga utachezeshwa kwa msaada wa VAR.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Yanga kuchezeshwa kwa msaada wa Video Asistance Referee VAR.

Kutokana na jambo hilo kocha wa Yanga Nabi amewaonya wachezaji kuacha kucheza michezo faulo zisizo na ulazima kwani inaweza kuwaletea shida kutokana na uwepo wa VAR.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Fiston Mayele, Farid Mussa, Mudathir Yahya, Aziz KI.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: