Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiemtaka kaja, Simba wamtambulisha Luis Miquissone

Jose Asaini Jose Luis Miquissone

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya fununu za muda mrefu hatimaye leo Julai 22 Klabu ya Simba imemtambulisha nyota Jose Luis Miquissone kama usajili wao mpya kuelekea msimu mpya 2023/24.

Miquissone amesajiliwa na Simba akitokea kwa Mabingwa wa Misri, Klabu ya Al Ahly aliyoachana nayo siku chache zilizopita kwa makubaliano ya pande mbili.

Miquissone amesaini Mkataba wa miaka miwili na Simba SC utakaofika tamati mwaka 2025.

Miquissone aliwahi kucheza Simba kwa mafanikio makubwa kabla ya kuuzwa kwa pesa ndefu kwenda kwa Mafarao wa Misri ambako huko hakuwa na mchezo mzuri na baada ya misimu miwili ameamua kuja kujiunga na waajiri wake wa zamani.

Miquissone anatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kuelekea nchini Uturuki kujiunga na kambi ya Simba iliyopo Uturuki.

Swali ni Je nani anatoka kupisha nafasi ya Jose Luis Miquissone kwa sababu tayari Simba ina wachezaji 12 wa Kimataifa mpaka hivi sasa.

Tupe maoni yako Mwanasimba nani aoneshwe mlango wa kutokea ili kumpisha Miquissone?

Je usajili huu wa Miquissone umeupokeaje, Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: