Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiemtaka kaja! Simba waifuata Yanga Fainali Ngao ya Jamii

IMG 5304.jpeg Moses Phiri na Ally Salim wakishangilia ushindi

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wekundu wa msimbazi, Timu ya Simba SC wamefanikiwa kupenya hatua ya Fainali Ngao ya Jamii 2023 baada ya kuichapa Klabu ya Singida Faountain Gate Mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Simba wanakwenda Fainali kwa ushindi wa penati 4-2 baada ya dakika 90 za mtanange huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Wachezaji wa Singida FG, Aziz Andambwile na Yusuph Kagoma walikosa mikwaju yao ya penati huku Luis Miquissone, Saido, Mzamiru Yassin na Moses Phiri wakipachika mikwaju yao ya penati.

Mlinda mlango wa Simba chipukizi Ally Salim ameibuka shujaa baada ya kuokoa mkwaju wa Penati ya kiungo wa Singida, Andwambile.

Kwa ushindi huo Simba wanakwenda kukutana uso kwa na mtani wake wa Jadi timu ya Yanga ambao nao walifanikiwa kutinga Fainali baada ya kuiondosha Azam FC kwa mabao 2-0.

Mchezo wa Fainali ya Ngao ya Jamii 2023 utapigwa Jumapili Agosti 13 saa moja usiku Uwanja wa Mkwakwani.

Je Simba watavunja uteja wa kuchapwa mara mbili mfululizo na Yanga? Au Yanga wataendelea kumfanya Simba kibonde? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: