Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuwaheshimu Djuma Shabni na Yanick Bangala

Yanga Djuma Bangala 50 Djuma Shabni na Yanick Bangala.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naamini unakumbuka ujio wake wachezaji Yannick Bangala na Juma Shabani wakitokea AS Vita ya DR Congo.

Bila shaka ni kati ya wachezaji wa kigeni wamekwenda kuwa mfano mkubwa wanapokuwa kazini.

Bangala amebeba MVP wa Ligi Kuu Bara ya @nbc_tanzania Djuma ameonyesha ni beki bora wa kulia na ndiye pekee ametikisa ufalme wa Shomari Kapombe akitokea pembeni kulia.

Uzoefu wao ni mkubwa, fainali ya Ligi ya Mabingwa, mara mbili wakiwa na AS Vita na wamekwenda fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa na Yanga, si jambo dogo.

Ninaamini ni wachezaji wanaopaswa kupewa heshima yao na nasema hivi kwa kuwa nimeona baadhi ya mashabiki wanawaona kama wasaliti na kusema maneno yasiyofaa dhidi yao.

Hawa wanastahili heshima na kama ni suala la kutaka kuondoka kwenye TETESI ZA USAJILI kila mmoja anaweza kuwa kapokea habari tofauti.

Nilizopata mimi ni kuwa Bangala na Shabani hawana mpango wa kuondoka Yanga ila klabu inataka kuwapeleka kwa mkopo Singida Fontaine Gate, jambo ambalo hawalitaki.

Mkataba wao umebaki mwaka mmoja, wao wanaomba waachwe kwa kuvunjiwa mkataba au wabaki na si kupelekwa kwa mkopo.

Hofu wakiachwa wanaweza kuchukuliwa na timu za Tanzania jambo ambalo ndilo linazua mvutano.

Jambo jema kuwapa heshima yao ni kubaki nao au kuwaacha na si kuwabana kwa kuwa wamefanya kazi kubwa na wanastahili heshima.

Inawezekana umesikia tofauti na mimi lakini kumbuka kuwashambulia kabla ya kupata uhakika unaweza kuwa sehemu ya kuwakandamiza bila kujua.

Tuuachie uongozi wa klabu yao, tuamini wanaweza kutenda SAHIHI na kama wanaondoka wakapewa UHURU na kama wanabaki wakapewa USHIRIKIANO.

Halafu baada ya TETESI ZA USAJILI, tutaweza kuzungumza mengi yenye uhakika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: