Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tshabalala afunguka kuhusu kutemwa Timu ya taifa

Amreach Kapombe Tshabalala Tshabalala afunguka kuhusu kutemwa Timu ya taifa

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: Nipashe

Nahodha Msaidizi wa Klabu ya Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' amesema maongezi waliyoyafanya na Kocha mpya wa Taifa Stars, Adel Amrouche akiwa na Shomari Kapombe baada ya mechi ya Simba dhidi ya Horoya yatabaki kuwa siri yake.

Tshabalala amefunguka hayo kufuatia maneno mengi kusambaa mitandaoni huku kukiwa na mjadala kuhusu kwa nini Kocha huyo aliwaacha wakongwe hao.

“Yule ni Mwalimu na anapokuwa kuwa ni Mwalimu ni zaidi ya Mzazi, tuliyozungumza yanabaki kuwa siri yangu...”

Kuhusu kuachwa kwenye Timu ya Taifa, Tshabalala amesma; “Ile ni National Team Mtu akiitwa ni kwa ajili ya kwenda kupambania Taifa, waliokuwepo wanapambania Taifa, Mimi ni Mtanzania kama muda wangu utakuwepo na nami nitapambania, nipo nyuma yao wapo vitani nawa-support.”

Shomari Kapombe na Mohammed Hussein ni miongoni mwa Wachezaji ambao hawajaitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa (Taifa Stars) kitachocheza na Uganda siku ya kesho kuwania kucheza AFCON.

Chanzo: Nipashe
Related Articles: