Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Top 25: Simba, Yanga zapanda viwango vya ubora CAF, zaandika rekodi

Simba Yanga Caf Rank Top 25: Simba, Yanga zapanda viwango vya ubora CAF, zaandika rekodi

Tue, 4 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu za Simba na Yanga zimepanda katika viwango vya ubora kwenye michuano ya CAF baada ya kukamilika kwa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la Shirikisho.

Klabu ya Simba imepanda kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 11 mpaka nafasi ya 7.

Simba ni miongoni mwa timu nane zilizofuzu robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa wakisubiri droo ya mechi za robo fainali itakayopigwa Jumatano huko Misri.

Yanga imepanda kwa nafasi 26 kutoka nafasi ya 46 mpaka nafasi ya 20 baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho.

Kwa mara ya kwanza Yanga imeingia katika klabu 20 bora barani Afrika. Wananchi wanaweza kusogea juu zaidi kama watafanikiwa kuvuka hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: