Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Timu bora imepoteza - Mchambuzi

Yanga Mwed Ngao Timu bora imepoteza - Mchambuzi

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukweli mchungu ambao bila shaka utakubaliwa na mashabiki wa Simba SC ni kuwa, Yanga Sc wamewaacha hatua kadhaa kwa ubora wa timu.

Yanga wako mbali ukilinganisha na timu nyingi za Tanzania. Wakijipata kwenye finishing timu nyingi zitataabika, zitafungwa magoli mengi kwa sababu wachezaji wabunifu wameongezeka kikosini wanatengeneza nafasi nyingi.

Yanga -------------- Simba

01 ....... On target ....... 01

05 ....... Off target ...... 01

07 ......... Corner ........ 01

13 ......... Fouls ......... 13

06 ........ Off-side ....... 00

00 ..... Yellow cards ...... 02

56 ....... Possession ...... 44

◉ Yanga wangekuwa na mshambuliaji mzuri kuanzia mwanzo leo wangeshinda si chini ya goli (3).

Timu nzima imeunganika vizuri limebaki eneo moja tu kwenye finishing. Gamondi anapaswa amuamini Konkani aache kujaribu wachezaji. Mzize ni mchezaji mzuri ila si wa kuwa chaguo la (1) kikosini. Musonda pia anapaswa kujitafakali.

◉ Simba SC wachezaji wengi wanacheza kwa uwezo binafsi, hakuna muunganiko na level ya fitness iko chini. Ukiona michezo miwili mfululizo golikipa ndio anaibuka kuwa Man of the match ujue kuna tatizo mahali.

Ukiamua kuichambua zaidi Simba na kuacha ubora wa Yanga utakuwa umeamua tu, ukichagua kuzungumza mambo mengi bila kutaja ubora wa mikono ya Ally Salim basi umeamua tu.

Yanga kupoteza Ngao kwa penati kwakuwa Simba walikuwa bora sana, upigaji mzuri na utulivu umewapa ushindi, hakuna kingine zaidi ni mpira wa miguu unakupa kwa kadri ulivyojipanga.

Yes upigaji kwa Wachezaji wa Yanga haukuwa mzuri kwenye penati! Yes ni mechi nzuri sana kwa Yanga kufahamu madhaifu yao na kuyafanyia kazi.

Kupoteza kwa Yanga kwa penati ni ahueni kubwa kwa Robertinho kwa jinsi Simba ilivyozidiwa uwanjani kwa kila kitu leo, ingetokea Yanga akashinda nadhani kibarua chake kingekuwa matatani. Timu bora kiwanjani imepoteza mchezo. Timu yenye bahati imeshinda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: