Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Thank you' Simba, Yanga, Azam zilivyotikisa

Nabi Fei Morrsion ‘Thank you' Simba, Yanga, Azam zilivyotikisa

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ilikuwa ni wiki ya aina yake kwa mashabiki wa soka nchini, wakati klabu kubwa nchini, Simba, Yanga na Azam FC zilipokuwa zikitoa mkono wa kwa heri kwa wachezaji, makocha na watu wa mabenchi ya ufundi.

Ni kama zilikuwa zinashindana hivi kutoa taarifa hizo kwenye mitandao yao ya 'Instagram'. Huyu akitoa hii na mwingine anatoa ya kwake.

Wakati mwingine sasa ikawa kama burudani hivi kwa mashabiki wa wasomaji, na kama kawaida ya Watanzania, utani ukawa mwingi kwenye mitandao ya kijamii.

Neno lililokuwa likitumiwa zaidi kama kichwa cha habari ni la kiingereza 'Thank you' na baada ya hapo inafuata taarifa ya kuachana na wanaowaacha.

Simba na Azam ndiyo zilizotia fora kwa kuagana na wafanyakazi ke wake wengi, tofauti na Yanga ambapo wao wameachana na wawili tu.

Simba yenyewe ilitia fora kwa kuchapisha 'thank you' kila baada ya muda mfupi kwa siku moja, tofauti na Azam ambayo angalau ilikuwa ikifanya hivyo kila baada ya siku moja.

Neno 'thank you' likaanza kuwa maarufu kwa mashabiki wa soka ambao kwa sasa wameanza 'kumiss' soka baada ya msimu wa mashindano kumalizika. Burudani yao sasa ikawa ni kwenye mitandao ya kijamii kujadili posti hizo.

Na utani mwingi ukaendelea, wengine wakaenda mbali kuwa mwisho wanaweza kuona posti za 'thank you' kwa wachezaji, makocha na viongozi ambao ndiyo muhimili wa klabu zenyewe. Huo ni utani tu.

Lakini kwa mujibu wa viongozi wa klabu hiyo, lengo ni kuondoa baadhi ya watu na kuleta wengine kwa ajili ya maboresho wa timu zao kwa msimu ujao wa ligi.

Ni Yanga tu ndiyo makocha wao wameondoka kwa sababu ya kumaliza mikataba, huku wao wakitaka kuwaongeza, lakini ikashindikana.

Mwandishi wa makala haya amekusanya taarifa za wachezaji, makocha walioondoka au kuachwa na klabu hiyo.

1. Nasreddine Nabi-Yanga Yanga ilikuwa inamhitaji sana kocha huyu aendelee kubaki na sababu zinaeleweka kwa kila mtu kwani ndiye kinara wa mafanikio ya misimu miwili mfululizo, hasa huu.

Viongozi wa klabu hiyo walijitahidi kutaka kumbakisha, lakini baada ya mazungumzo marefu ilishindikana.

Nabi ameondoka Yanga na taarifa zinasema klabu ambayo huenda akatua ni Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, na huenda akaondoka na robo tatu ya benchi lake ya ufundi.

2. Chlouha Zakaria-Simba 'Thank you' za Simba ilianza kwa kocha wa magolikipa, Chlouha Zakaria raia wa Morocco. Alijiunga na Simba Novemba mwaka jana, lakini ni mmoja wa watu walioachwa ili kupisha maboresho.

3. Bruce Kangwa-Azam FC Mpaka sasa ni Azam pekee ambayo 'thank you' zake zimelenga mpaka kwa wachezaji. Zimemgusa nahodha wa klabu hiyo Mzimbabwe Bruce Kangwa ambaye amepewa mkono wa kwa heri. Alisajiliwa na timu hiyo mwaka 2016 akitokea nchini Zimbabwe.

4. Kelvin Mandla-Simba Huyu ni kocha wa viungo wa klabu ya Simba raia wa Afrika Kusini. Naye alijiunga Novemba mwaka jana kwa mkataba wa mwaka mmoja. hata hivyo ni mmoja wa walioachwa msimu huu, akipigiwa kelele na wanachama na mashabiki wengi kuwa ameshindwa kuwafanya wachezaji kuwa na stamina na pumzi.

5. Milton Nienov - Yanga 'Thank you' nyingine kati ya nyingi wiki hii, ilikwenda kwa kocha wa magolikipa wa Yanga ambaye yeye amemaliza mkataba wake kwenye klabu hiyo. Awali alifanya kazi kwenye klabu ya Simba.

6. Kenneth Muguna - Azam FC Ni kiungo mkabaji raia wa Kenya, ambaye Azam imeamua kuachana naye na kumwambia 'thank you', kwa kazi nzuri aliyoifanya huko nyuma.

Alisajiliwa 2021 akitokea klabu ya Gor Mahia ya Kenya, hivyo hatokuwa sehemu ya timu hiyo msimu ujao.

7. Fareed Cassim-Simba Ni mtaalam wa viungo na misuli wa klabu hiyo ambaye ni Simba wameamua kuachana naye, sababu kuwa ikiwa ni kuumia mara kwa mara kwa wachezaji, lakini pia wanachelewa kupona, hivyo sehemu hiyo ni moja kati ya sehemu ambazo Simba wanataka kuboresha. Alishawahi kufanya kazi Yanga.

8. Rodgers Kola-Azam FC Straika huyu raia wa Zambia naye amepewa mkono wa kwa heri, akiwa amejiunga na klabu ya Azam FC 2021, akitokea Zanaco ya nchini humo.

9. Cleophace Mkandala-Azam FC Kiungo huyo alisajiliwa na Azam mwaka jana, ikiipiku Simba katika kinyang'anyiro cha kumuwania kutoka Dodoma Jiji, lakini leo hii ni mmoja wa wachezaji waliopewa 'thank you', ili kupisha wengine kuendeleza jahazi.

10. Ismail Aziz Kada-Azam FC Azam FC ilimsajili winga huyu kutoka Prisons mwaka 2020 akiwa kwenye kiwango cha juu na aliisaidia kwenye mechi za msimu uliopita. Msimu huu yupo kwenye orodha ya walioonyesha mlango wa kutokea.

11. Kalimangonga Ongalla-Azam FC Pamoja na kucheza mechi 32, akiiongoza kushinda 21, sare nne na kupoteza saba, lakini Azam FC imeona haitoshi, ikampa mkono wa kwa heri, kocha wake na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Kalimangonga Ongalla.

12. Aggrey Morris-Azam FC Azam ikaendelea kushangaza wengi ilipompa 'thank you' nahodha wake wa miaka mingi, Aggrey Morris ambaye hadi wanaachana naye alikuwa kocha msaidizi wa timu hiyo.

13. Wibol Maseke-Azam FC Kwa kuonyesha kuwa imedhamiria kusafisha, Azam FC imempa mkono wa kwa heri mchezaji ambaye ilimlea yenyewe kwenye kituo chake cha kukuza vipaji na kumpandisha msimu wa 2019, Wibol Maseke. Sasa yupo huru kwenda timu yoyote ile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: