Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takwimu za Mamadou Doumbia mechi ya kwanza Yanga

Mamadou Doumbia Ty Takwimu za Mamadou Doumbia mechi ya kwanza Yanga

Thu, 13 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi juzi Aprili 11, 2023 alimtumia kwa mara ya kwanza beki Mamadou Doumbia katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Doumbia aliingia dakika ya 67 kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika uwanja wa Azam Complex

Doumbia alitumia takribani dakika 25 alizotumika katika mchezo huo akionyesha umahiri wake katika kupiga pasi, kunusa na kuokoa hatari pamoja na kucheza mipira ya juu

Mara kadhaa Nabi aliweka bayana kuwa Doumbia hatumiki sio kwa sababu ni mchezaji mbaya, bali anampa muda ili aweze kuzoea mbinu ya aina ya uchezaji wa wenzake

Wakati Doumbia anasajiliwa na Yanga, tayari aliwakuta wenzake wanafanya vizuri katika nafasi anayocheza hivyo ilikuwa ni lazima kwa Nabi kuwa na uvumilivu ili kuhakikisha hamuweki kwenye presha kubwa

Taratibu Doumbia ameanza kuonekana na bila shaka wale waliokuwa na mashaka nae watatulia.

Takwimu zake;

Dk. 23

25. Touches

10(10) passes

100% pass accuracy

01. Clearances

00. Blocks

01. Aerial Duels | high boll’s Won

Umekionaje kiwango cha Mamadou Doumbia Kwenye mchezo huo?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: