Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TETESI: Simba kushusha Mbrazil nafasi ya Manula

IMG 4415.jpeg Caique Luiz Santos da Purificacao (25)

Sat, 24 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimu ujao pale langoni Simba kitasimama chuma cha Kibrazil Caique Luiz Santos da Purificacao (25).

Kama mipango itaenda sawa basi kipa huyo ndiye atakayechukua nafasi ya Aishi Manula ambaye vipimo vinaonyesha atachelewa kurejea.

Manula alipata majeraha yaliyompelekea kufanyiwa upasuaji huku Mlinda mlango namba mbili Beno Kakolanya akioneshwa mlango wa kutokea baada ya Mkataba wake kumalizika.

Caique Luiz Santos da Purificacao alikuwa kipa namba moja wa kikosi cha Brazil wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 (Brazil U-20) mwaka 2016 na 2017.

Kwa sasa Simba imebakiwa na mlinda mlango Ally Salim pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: