Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Yanga ageukia kilimo

Nchimbi Tre Straika Yanga ageukia kilimo

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa soka wa zamani wa klabu ya Yanga, Azam FC na zingine nyingi, Ditram Nchimbi (26) amegeukia shughuli ya Kilimo baada ya kuachana na klabu ya Fountain Gate inayoshiriki Ligi ya Championship.

Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Nchimbi amesema kuwa maisha ya Kilimo ameyakuta na ndiyo yaliomkuza mpaka watu kumfanya waamfahamu katika soka.

“Nimezaliwa na kuyakuta haya maisha ndiyo yalinikuza na nikawa huyu Ditram unayemfahamu wewe kwa vile unamfahamu na kumuona ulikomuona” aliandika

Nchimbi ameendelea kwa kuwakaribisha watu mbalimbali katika mkoa wa Tunduru; ”Karibuni Tunduru mengine ni baraka za Mungu ila tumetoka huku”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: