Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu hati hati kuikosa Fainali Jumapili

Skudu Raha Winga wa Yanga, Skudu Makudubela

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga SC, Skudu Makudubela anaendelea vizuri kwa sasa baada kupata jeraha na kutolewa nje dakika ya saba (7) kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC Agosti 9 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.

Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga SC, Walter Harrison amesema Skudu anaendelea vizuri japo kucheza mchezo wa Fainali dhidi ya Simba SC bado ni asilimia 50/50.

Walter amesema kwa sasa Skudu hafanyi mazoezi na wenzake na badala yake yupo chini ya uangalizi maalum wa Timu ya Madaktari, lakini akaongeza kuwa kutokuwepo kwa Skudu hakutapunguza kitu kwani Winga Jesus Moloko anarejea kikosini.

Je Mwananchi una lolote la kuzungumza?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: