Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu amekuja Yanga kula pensheni - Jemedari Said

Skudu Makudubela.jpeg Skudu Makudubela.

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi maarufu wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said Kazumari amesema kuwa, winga mpya wa Yanga SC, SKudu Makudubela amekuja nchini kula pensheni kwani umri wake ni wa kustaafu soka wakati wowote.

Usiku wa kuamkia jana Julai 19, 2023, Klabu ya Yanga ilimtambulisha nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 raia wa Afrika Kusini akitokea Marumo gallants ya nchini mwao ili kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho.

Skudu anafahamika kwa umahiri wake wa kupiga chenga, kuchezea mpira na kuwavuruga mabeki wa wapinzani pale anapokutana nao dimbani kwa umachachari wake.

"Ni mchezaji Mkongwe katika Ligi ya South Africa amecheza PSL Ligi Kuu miaka 13 toka akiwa na miaka 20 wakati huo sasa ana miaka 33 anatumia Mguu wa kushoto ni mchezaji mzuri mwenye umbo dogo anaejua kucheza na Mpira vizuri mtindo unaopendwa sana South Africa.

"Katika misimu sita ya nyuma Kila msimu amekuwa na Timu mpya mfululizo toka mwaka 2016 mpaka sasa na kukaa misimu miwili bila timu akiwa na Majeraha.

"Msimu uliopita Alisajiliwa na Timu ya Marumo na kucheza kwa mafanikio sana katika Confederation Cup na upande wa ligi Timu iliweza kushuka Daraja toka PSL na yeye akawa huru kuchagua kwa kwenda msimu huu.

"Hivyo sasa SKUDU MAHLATSI MAKUDUBELA ni FREE AGENT anatafuta malisho popote pale ndani na nje ya South Africa kama PENSHENI. BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)," amesema Jemedari Said Kazumari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: