Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Skudu aanza na balaa hili kwa Mkapa, GSM apagawa(+Video)

Skudu X GSM Skudu aanza balaa kwa Mkapa, GSM apagawa

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati akisifika kama Waziri wa raha na burudani katika kikosi cha Dar Young Africans.

Mchezaji mpya katika kikosi hicho Mahlatse Makudubela "Skudu" amethibitisha hilo mbele ya macho ya wengi wakati wa kilele cha Tamasha la "Siku ya Mwananchi" leo Julai 22 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Wakati akitambulishwa kama mchezaji wa Yanga kuelekea msimu ujao 2023/24, Skudu alipewa mpira akafanya vitu vyake na kuibua shangwe kubwa kwa wapenzi wa Yanga waliofurika Uwanjani hapo.

Mbali na hilo Mwekezaji wa Klabu ya Yanga GSM alijikuta akifurahi na kupiga makofi, Rais wa Yanga hali kadhalika Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro alijikuta akifurashishwa na "mavituz" ya Skudu.

Tazama Video hapa chini na utuambie una matarajio gani na winga huyo mpya ambae atacheza mchezo wake wa kwanza leo katika jezi ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: